slider gif

slider gif

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

kilimanjaro CAN ONLY B CLIMBED FROM TZ

Wednesday, December 13, 2017

WAZIRI KIGWANGALLA AFAFANUA KUHUSU KAMATI YA KITAIFA YA KUANDAA UTAMBULISHO WA TANZANIA


TAARIFA KUHUSU KAMATI YA UTAMBULISHO WA TANZANIA (DESTINATION TANZANIA BRANDING COMMITTEE)

Salaams, 

Siku chache zilizopita mimi, Hamisi Kigwangalla, katika kutekeleza 
majukumu yangu kama Waziri wa Maliasili na Utalii, niliteua kamati ya Kitaalamu ya watu waliobobea kwenye mambo ya ubunifu wa mikakati ya masoko, 
mawasiliano, mahusiano kwa umma, utalii na biashara. Lengo kuu likiwa kuanzisha mchakato
wa kitaalam (technical) wa kuandaa utambulisho mpya wa Tanzania kwenye masoko ya kimataifa ya Utalii. Kamati hii inakusudiwa kufanya uchambuzi wa kina wa tafiti mbalimbali na kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali muhimu kisha kuniletea mapendekezo yao. 

Kwa kuzingatia ukweli kwamba, Maliasili na Utalii siyo Wizara ya Muungano na kwamba utalii, kimsingi ni katika mambo yatakayodumisha zaidi Muungano wetu na Umoja wetu, sababu kimkakati na kiutekelezaji hatuwezi kukwepana, na kwamba uuuzaji wa vivutio vya utalii ni katika mambo ya kufanywa kwa pamoja ili kuwa na tija kwa Taifa letu, nilipokea ushauri kwamba ni vema toka hatua za awali tuweke wajumbe wanaotokea Zanzibar, kwenye Kamati hii. 

Awali tulikuwa na fikra kwamba baada ya kazi za mwanzo kufanyika na kuwa na andiko la kitaalamu (technical proposal) la kufanyia kazi, tungeanzisha mawasiliano rasmi ndani ya Serikali zetu mbili, ambapo kungekuwa na majadiliano ngazi ya wataalam na baada ya hapo ngazi ya Mawaziri. Mpango huu bado tunao. 

Tumekuwa na utamaduni wa kufanya kazi pamoja na kwa ukaribu kwenye kutangaza vivutio vilivyopo sehemu zote mbili za Muungano na tutaendelea kufanya hivyo. Watalii wanaokuja kwenye mbuga hupenda kwenda Zanzibar kufanya utalii wa fukwe na wa kiutamaduni, na kinyume chake. Hivyo, hatuwezi kukwepa kufanya kazi pamoja.

Mimi binafsi ni muumin mkubwa na mahiri wa Muungano, na utangamano kwa ujumla wake. Pia ni muumin mkubwa wa ushirikishwaji kama zana muhimu ya kufanyia maamuzi nyeti, siwezi kuwa wa kwanza kukiuka msingi wa imani yangu kama kiongozi. Hatua stahiki itakapofika tutakaa na Waziri pacha wa Utalii wa Zanzibar kushauriana na kukubaliana. 

Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB. 
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII.

No comments:

Post a Comment